Breaking

for more information click below

PropellerAds

Thursday, 13 June 2019

TATIZO LA KISUKARI (DIABETES MELLITUS)

PropellerAds
TATIZO LA KISUKARI (DIABETES MELLITUS) 0692385087/0765044875
Miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu wa nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania ni ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa huu hutokea pale ambapo tezi kongosho linaposhindwa kutengeneza kichocheo aina ya Insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha sukari kwenye damu au hyperglycemia.
Aina za Kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo
1)Aina ya kwanza ya Kisukari au Type 1 Diabetes Mellitus
PropellerAds
Hii ni aina ya kisukari inaawaathiri zaidi watoto na vijana (young adults). Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans katika tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.
Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa kwa tezi kongosho kunakoweza kufanywa na magonjwa ya kinga ya mwili wa mtu mwenyewe au autoimmune diseases; au kushambuliwa na vyanzo visivyojulikana yaani idiopathic causes.
2)Aina ya pili ya Kisukari au type 2 Diabetes Mellitus
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua kwa ufanisi utendaji kazi wa homoni ya insulin.
PropellerAds
Hali hii husababishwa na unene uliopitiliza yaani obesity, au hali ya kutofanya mazoezi kabisa (physical inactivity). Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa katika kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi wa utendaji kazi wake, wagonjwa wa aina hii ya kisukari hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. Ndiyo maana aina hii hujulikana pia kama kisukari kisichotegemea insulin au Non Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM)
3)Kisukari cha Ujauzito (Gestational DM)
Ni aina ya kisukari kinachotokea pindi kunapokuwa na ongezeko la kiwango cha sukari katika damu (hyperglycemia) wakati wa ujauzito. Aina hii ya kisukari huathiri karibu asilimia 2-5 ya mama wajawazito wote ingawa wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua. Hata hivyo karibu asilimia 20 mpaka 50 ya mama wajawazito wanaopata aina hii ya kisukari huweza kuendelea nacho hatimaye kuwa aina ya pili ya kisukari au type 2 DM maishani.
Dalili za Kisukari
PropellerAds
Kukojoa mara kwa mara (polyuria)
Mgonjwa kujihisi kiu kikali na kunywa maji kupitiliza (polydipsia)
Mgonjwa kujihisi njaa na kula mara kwa mara (polyphagia)
Kuchoka haraka (easy fatiguability)
Kupungua uzito
Vipele mwilini ambavyo kitaalamu huitwa diabetic dermadromes
Wagonjwa wa kisukari pia huwa katika hatari ya maambukizi katika kibofu cha mkojo, ngozi na kwa wanawake sehemu za siri.
Aidha kuna dalili maalum ambazo hutokea kwa wagonjwa wa kisukari iwapo mgonjwa atapatwa na mojawapo ya madhara (complications) ya ugonjwa huu. Madhara (complications) haya hujulikana kama Diabetic Ketoacidosis na Hyperosmolar non-ketotic coma. Diabetic Ketoacidosis au kwa kifupi DKA hutokea kwenye aina ya kwanza ya kisukari (type 1 DM), nayo huwa na dalili zifuatazo
Mgonjwa hutoa harufu ya acetone (inafanana kiasi na harufu ya pombe)
Mgonjwa hupumua kwa haraka na kwa nguvu, hali hii huitwa Kussmaul's breathing
Kujihisi kichefuchefu
Kutapika
Kujihisi maumivu ya tumbo na
Kupoteza fahamu.
Hyperosmolar Non-ketotic coma hutokea kwenye kisukari cha aina ya pili (type 2 DM). Hali hii mara nyingi husababishwa na upungufu wa maji mwili (dehydration) na mgonjwa huweza kupoteza fahamu.
Madhara ya Kisukari
PropellerAds
Kuziba kwa mishipa mikubwa ya damu, Mgonjwa kushindwa kuona vizuri au kushindwa kuona kabisa na kuwa kipofu, Kushindwa kufanya kazi vizuri kwa figo, Kupungua kwa nguvu za kiume, Vidonda (diabetic ulcers) hususani vidoleni, Mgonjwa kuhisi ganzi na kupoteza kuhisi mikononi na miguu, Mgonjwa kuwa hatarini kupata maambukizi ya vimelea mbalimbali hasa bacteria
Kwa matibabu ya tatizo hili kwa kutumia Tibalishe na virutubisho (food supplements) wasiliana nasi kwa namba 0692385087/0765044875. Tunapatikana Kinondoni-Morocco, Dar es salaam. Pia tunatoa huduma ya vipimo vya mwili mzima (full body checkup) kwa Tsh 10,000/= tuu.
PropellerAds
NB:
BOFYA hapa CHINI kupata mfululizo wa makala yetu ya afya kila siku
Facebook page https://www.facebook.com/allyhamisi1225/
Whatsapp group https://chat.whatsapp.com/CwoN9qKG1wu6Rh8LgPTrxV
Instagram page @allyhamisi_ @allyhamisi_
PropellerAds

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

PropellerAds