HEDHI: VIASHIRIA SITA (6) VYA KUMUONA DAKTARI
Ni kawaida kwa mwanamke kuona siku zake kila mwezi. Lakini je, utajuaje kama hedhi anazopata mwanamke ni kawaida au kuna tatizo?
Kwa kawaida, hedhi huchukua wastani wa siku 2 hadi 7. Mzunguko wa hedhi kwa wastani ni wa siku 28, ingawa pia ni kawaida kuwa na siku kadhaa pungufu au zaidi.
Baadhi ya mabadiliko ya hedhi yanayoweza kuashiria kuwa kuna tatizo ni yafuatayo :
Kutokuona siku zako / Kuruka mzunguko wa mwezi
Mara nyingi hii hutokea kama mwanamke amepata ujauzito. Kama umekuwa na mahusiano ya karibu na mwenzi wako katika kipindi cha karibu, waweza kupima mkojo kuona kama una ujauzito. Pia, fika katika kituo chetu cha afya Eternal Inyernational kwa ajili ya vipimo zaidi.

Aidha, hii inaweza pia kusababishwa na msongo wa mawazo, kupungua uzito kwa ghafla, unene uliopitiliza, kufanya mazoezi kupita kiasi, utumizi wa vidonge vya uzazi wa mpango, umri zaidi ya miaka 49, na baadhi ya magonjwa katika mfumo wa uzazi.
Kutokwa na damu kabla ya siku zako / baada ya tendo la ndoa
Hii yaweza kutokana na maambukizi ya vijidudu, matatizo ndani ya mfumo wa uzazi au saratani. Pia kwa watumiaji wa tiba ya vichocheo katika miezi 3 ya Kwanzaa
Hii yaweza kutokana na maambukizi ya vijidudu, matatizo ndani ya mfumo wa uzazi au saratani. Pia kwa watumiaji wa tiba ya vichocheo katika miezi 3 ya Kwanzaa
Kutokwa na damu nyingi au kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida
Hii yaweza kusababishwa na saratani ya mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi au mabadiliko yanayotangulia saratani.
Hii yaweza kusababishwa na saratani ya mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi au mabadiliko yanayotangulia saratani.
Kuona siku zako baada ya kutimiza umri wa kuacha (menopause)
Si kawaida kwa mwanamke aliyetimiza umri, kuendelea kutokwa na damu zaidi ya miezi 12 baada ya kuacha kuona siku zake. Yaweza kuwa kwa sababu ya saratani ya mfuko wa uzazi, mlango wa mfuko wa uzazi (cervix), saratani katika uke (vagina) n.k.

Kutokwa na uchafu wakati wa hedhi
Uchafu huu unaweza ukawa unatoa harufu, wa rangi ya kijani au umechanganyika na damu. Hii yaweza kuashiria uwepo wa maambukizi.
Uchafu huu unaweza ukawa unatoa harufu, wa rangi ya kijani au umechanganyika na damu. Hii yaweza kuashiria uwepo wa maambukizi.
Maumivu makali sana (yasiyo ya kawaida) wakati wa hedhi
Yaweza kusababishwa na uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (fibroids), seli za mfuko wa uzazi kuota nje ya mfuko wa uzazi (endometriosis) pamoja na magonjwa mengine. Pia, yaweza kutokuwa na sababu yeyote dhahiri.
Hedhi yaweza kubadilika. Mabadiliko haya sio mara zote humaanisha kuna tatizo, lakini ni muhimu kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi ili kuwa salama.
Eternal International tunatoa huduma ya vipimo vya mwili mzima (full body checkup) kwa gharama ya tsh 10,000/= tuu, pamoja na matibabu ya matatizo ya uzazi ma mengine sugu kwa kutumia dawa (Virutubisho) zenye uwezo wa kuondoa tatizo na kuweka kinga. Wasiliana nasi kwa namba 0692385087/0765044875. Tunapatikana Kinondoni-Morocco, Dar es salaam
@allyhamisi_ @allyhamisi_
NB:
BOFYA hapa CHINI kupata mfululizo wa makala yetu ya afya kila siku
Facebook page https://www.facebook.com/allyhamisi1225/
Whatsapp group https://chat.whatsapp.com/CwoN9qKG1wu6Rh8LgPTrxV
Instagram page @allyhamisi_ @allyhamisi_

No comments:
Post a Comment