UFAHAMU UGONJWA WA KIHARUSI (STROKE)
Kiharusi kinampata binadamu baada ya eneo la ubongo kukosa damu kwa saa 24 ama zaidi au kunapotokea kizuizi cha damu au mishipa ya damu kushindwa kusafirisha damu au mshipa huo unapopasuka.
Tatizo hili linalotokea ghafla kwenye ubongo ambapo mtiririko wa damu kwenye eneo fulani la ubongo husitishwa ghafla au kupungua sana hivyo kusababisha eneo hilo la ubongo kukosa damu na virutubisho muhimu na seli za eneo hilo kuanza kufa. Hili linaweza kutokea pale mishipa ya damu ya kuelekea kwenye eneo hilo ikiziba au mishipa ndani ya ubongo katika eneo hilo kupasuka. Seli za ubongo za eneo hilo zikianza kufa kwa kukosa damu, shughuli zote zinazoendeshwa na eneo hilo la ubongo husimama kwa mfano kumbukumbu au misuli.
Kiharusi ni ugonjwa wa dharura hivyo tiba inatakiwa ipatikane mapema iwezekanavyo. Kimsingi kiharusi huweza kumpata mtu ye yote wakati wo wote.
Kiharusi ni ugonjwa wa dharura hivyo tiba inatakiwa ipatikane mapema iwezekanavyo. Kimsingi kiharusi huweza kumpata mtu ye yote wakati wo wote.
AINA ZA KIHARUSI (STROKE)
Kuna aina tatu za stroke (i) Ischemic (ii) Hemorrhagic na (iii) TIA. Kundi la watu lililo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu ni lile la watu wenye miili mikubwa, umri zaidi ya miaka 55, wenye historia ya ugonjwa huu kwenye familia zao, ambao hawafanyi mazoezi , wanaokunywa sana pombe au kutumia madawa haramu.
KIHARUSI (STROKE) HUSABABISHWA NA NINI?
Tuangalie kila aina za stroke hapo juu na visababishi vyake:-
(i) Ischemic strokes: Hii ndiyo aina ya stroke inayowaathiri watu wengi zaidi, asilimia 85 ya wagonjwa wa stroke hupatwa na aina hii ya stroke. Aina hii ya stroke husababishwa na kuziba kwa artery (mishipa ya kusafirisha damu safi) zinazoelekea kwenye ubongo au kusinyaa kwa mishipa hiyo hivyo kusababisha hali inayoitwa ischemia (upungufu mkubwa wa mtiririko wa damu).
Kuziba kwa mishipa ya damu hutokea baada ya damu kuganda ndani ya arteri zinazoeleka kwenye ubongo au katika maeneo ya mbali zaidi na kusukumwa kwenye mishipa yenye kipenyo kidogo ndani ya ubongo. Mishipa hii inaweza kuzibwa pia na mafuta yaliyoganda ndani ya arteri (plaque).
(ii) Hemorrhagic strokes: Hii husababishwa na artery ndani ya ubongo kuvuja damu au kupasuka. Damu hii iliyovuja huleta mgandamizo kwenye seli za ubongo na kuziharibu. Kupasuka kwa mishipa ya damu husababishwa na hypertension, trauma au dawa zinazofanya mishipa hii ya damu kupungua unene wake.
(iii) Transient ischemic attack (TIA): Hiii ni tofauti na aina hizo mbili za stroke hapo juu kwani hapa mtiririko wa damu kuelekea kwenye ubongo huvurugwa kwa muda mfupi kwa sababu zile zile tulizozitaja hapo juu tulipozungumzia ischemic strokes. Stroke ya aina hii ni ishara ya kutokea strokes nyingine baadaye kama hatua zinazostahili hazitachukuliwa.
DALILI ZA KIHARUSI (STROKE)
Ugonjwa wa stroke humpata mtu ghafla na dalili hutokea kwa muda mfupi sana.
Dalili kuu za ugonjwa huu ni:-
Dalili kuu za ugonjwa huu ni:-
-Kuchanganyikiwa, mtu anapata shida ya kuongea na kuelewa anachoambiwa.
-Maumivu ya kichwa pamoja na kupoteza fahamu kwa vipindi na kutapika.
-Ganzi katika viungo vya uso, mkono na mguu na hasa vikiwa vya upande mmoja wa mwili.
-Kupata shida ya kuona kwa jicho moja au yote.
-Kupata shida ya kutembea, kuhisi kizunguzungu na kukosa mpangilio wa matendo ya mwili.

ATHARI ZA KIHARUSI (STROKE)
Athari za kiharusi zinaweza kuwa ni za muda mrefu Kulingana na muda uliopita kabla ya kuugundua na kuutibu ugonjwa huu, mtu anaweza kupata ulemavu wa muda mfupi au wa kudumu. Pamoja na madhara ya stroke kama yalivyoorodheshwa hapo juu, mgonjwa wa stroke anaweza pia kupata yafuatayo:-
i) Msongo wa mawazo
ii) Maumivu kwenye mikono na miguu yanayoongozeka baada ya viungo hivyo kufanya kazi au kutokea mabadiliko ya hali ya hewa.
iii) Kupooza au udhaifu wa upande mmoja wa mwili
iv) Kupata shida katika kufanya matendo ya kuonyesha hisia za mwili
v) Kushindwa kumudu matumizi ya kibofu cha mkojo au viungo vya njia ya haja kubwa.

TIBA ZA KIHARUSI (STROKE) NA NAMNA YA KUZUIA
Kwa vile Aina KUU Mbili za stroke, Ischemic na Hemorrhagic, kila moja ina chanzo kilicho tofauti, kila moja inahitaji tiba iliyo tafauti na ya aina nyingine. Ni shurti kujua kwa uhakika ni aina gani ya stroke iliyotambuliwa kwani tiba ya stroke ya aina moja inaweza kuwa na madhara kwa stroke ya aina nyingine.
(A)Tiba kwa Ischemic Stroke: Ischemic strokes hutokea pale mishipa ya damu inapoziba au kupungua kipenyo hivyo tiba ya tatizo hili ni kuhakikisha damu ya kutosha inaufikia ubongo. Tiba huanza kwa kotoa dawa za kuyeyusha damu au mafuta yaliyoganda na kuzuia hali hiyo isitokee tena.
(B)Tiba kwa Hemorrhagic stroke: Stroke ya aina hii hutokea pale damu inapovuja ndani ya ubongo hivyo tiba yake italenga katika kuzuia damu isiendelee kuvuja na kupunguza mgandamizo wa damu iliyovuja kwenye ubongo. Tiba huanza kwa kutoa dawa za kupunguza mgandamizo kwenye ubongo, kupunguza msukumo wa damu kwa ujumla na kuzuia kusinyaa kwa ghafla kwa mishipa ya damu. Upasuaji unaweza kutumika kurekebisha mishipa ya damu iliyopasuka .
ILI KUJILINDA NA KIHARUSI (STROKE) AU KUZUIA, YAFUATAYO YANAWEZWA KUFANYWA:-
-Kutotumia madawa haramu
-Kula chakula chenye mboga na matunda kwa wingi na chenye cholesterol kidogo
-Kufanya mazoezi kila wakati
-Kuhakikisha unadhibiti blood pressure
-Kuhakikisha unadhibiti kiwango cha sukari mwilini
-Kuwa una uzito unaofaa
-Kunywa pombe kwa kadri au kuacha kabisa
-Kuacha kuvuta sigara

Je, una tatizo hili au kuna unayemfahamu mwenye tatizo kama hili la Kiharusi (stroke) ? Na ungependa tuweze kuwasaidia? Usisite Kuwasiliana Nasi Kwa Namba 0692385087/0765044875. Tunapatikana Kinondoni, Morocco, Dar es salaam
Pia Tunatoa huduma ya vipimo vya mwili mzima (full body checkup) kwa Tsh 10,000/= Tuu
Ukihitaji huduma Piga/Tuma sms Usicomment
NB:
BOFYA hapa CHINI kupata mfululizo wa makala yetu ya afya kila siku
Facebook page https://www.facebook.com/allyhamisi1225/
Whatsapp group https://chat.whatsapp.com/CwoN9qKG1wu6Rh8LgPTrxV
Instagram page @allyhamisi_ @allyhamisi_

No comments:
Post a Comment