MAGONJWA YA FANGASI WA NGOZI NA MATIBABU YAKE (SUPERFICIAL MYCOSES)
Kuna aina milioni moja na nusu za wadudu aina ya fangasi wanaotambulika duniani, kati yao ni fangasi 300 tu wanaojulikana kusababisha maambukizi kwa binadamu. Uvutaji wa hewa iliyochanganyika na mazalia ya fangasi yanayojulikana kama fungal spores pamoja na uwepo wa uvamizi au ukuaji wa fangasi kwenye ngozi ya binadamu husababisha maambukizi ya fangasi, hivyo basi maambukizi mengi ya fangasi huanzia kwenye mapafu au kwenye ngozi ya binadamu.
Fangasi ni magonjwa yanayoathiri ngozi, kucha na nywele, pia huathiri mdomoni na sehemu za siri. Magonjwa haya huambukiza kwa njia ya kugusana au kushirikiana nguo hasa za ndani na taulo.
Fangasi ni magonjwa yanayoathiri ngozi, kucha na nywele, pia huathiri mdomoni na sehemu za siri. Magonjwa haya huambukiza kwa njia ya kugusana au kushirikiana nguo hasa za ndani na taulo.
Hapa tutaangalia fangasi katika kundi la magonjwa yanayoathiri ngozi, nywele na kucha (Dermatomycosis).
Kuna aina kuu tano (5) za magonjwa ya fangasi wa ngozi, nywele na kucha kama ifuatavyo:
1:Fangasi wa kichwani (Tinea Capitis)
Ugonjwa huu huanza na sehemu ndogo ya ngozi ya kichwa na kukua kuwa sehemu kubwa. Huathiri nywele na kuzifanya dhaifu, laini na nyepesi kukatika au kung'oka. Huwaathiri sana watoto chini ya miaka 10 na hupotea mtu akisha barehe.
2:Fangasi wa mwili (Tinea Corporis)
Ugonjwa huu hutokea mwilini, sehemu ya ngozi iliyoathiriwa huwa nyekundu, duara kama shiringi na kukua huku ikiacha sehemu ya katikati kuwa na ngozi nzuri. Maduara haya yanaweza kukaa yakiwa kadhaa katika sehemu moja ya ngozi.
3:Fangasi wa nyayo na vidole (Tinea Pedis (Athlete’s foot)
Ugonjwa huu hutokea kama mabaka na kuchanika katikati ya vidole na huwasha sana na kuuma pia.
4:Fangasi wa kucha (Tinea Unguium (Onchomycosis)
Ugonjwa huu huathiri kucha na hubadilisha rangi ya kucha. Huzalishwa vitu kama chaki na ambavyo vikisuguliwa huweza kupukutika. Kucha huweza kulika na inaweza kuisha.
5:Finea vesicolor (Pityriasis)
Huu ni ugonjwa wa fangasi ambao huathiri sehemu ya juu sana ya ngozi katika sehemu za usoni, shingoni na mgongoni. Hutokea kama viduara vyenye mng'ao vinavyo washa. Huongezeka na huathiri sehemu kubwa ya ngozi visipotibiwa ingawa vinaweza kupotea vyenyewe. Maranyingi ugonjwa huu hauambukizwi Ila hutokea kama ajari tu yanapotokea mabadiliko fulani ya mwili. Sio ugonjwa hari sana kiafya ila haukubaliki kwani huharibu mwonekano wa mtu hasa unapotokea maeneo ya uso na shingoni.
Tinea vesicolor (Pityriasis) huonekana sana kwenye ngozi ya watu wanaoishi sehemu zenye joto kali au wenye matatizo kwenye vichocheo vya miili yao (hormonal abnormalities) ingawa wote wanaopata maambukizi haya huwa ni watu wenye afya njema.

Huambukiza vipi?
Maradhi haya huambukiza kwa njia zifuatazo:
Kugusana na mtu mwenye maambukizi ya fangasi hawa
Kugusa vitu vilivyobeba fangasi wa aina hii kama vile nguo ikiwemo nguo za ndani, chanuo la nywele, mikufu, vifaa vya kuogea, viatu na soksi.
Unaweza kupata maambukizi pia kwa kugusa sehemu ambazo mwenye maradhi amegusa kama ukuta, viti, makochi na vitu vingine.

Dalili za maambukizi ni zipi?
Aina hii ya fangasi huwa na dalili chache sana na kubwa ni muonekano wake kama nilivyouelezea hapo juu. Ila vifuatavyo huonekana:
Kubadilika kwa rangi ya ngozi ya eneo lenye maambukizi, eneo la ngozi lenye maambukizi huwa lina muundo wa duara mfano wa sarafu ya fedha.
Ngozi kubanduka kwenye eneo lenye maambukizi pia kukauka kwenye eneo lenye maambukizi.
Inawezekana kabisa kupata muwasho kwenye eneo lililo na maradhi ingawa si sehemu zote za mwili zenye maambukizi zinaonyesha dalili hii.

Nani yupo hatarini?
Watu ambao huweza kupata maambukizi ya fangasi wa aina hii ni kama wafuatao:
Wale wanaofanya kazi zinazohusisha kugusana na watu wenye maambukizi ya fangasi wa aina hii
Wanaolala kitanda kimoja na wenye maambukizi ya fangasi wa aina hii Wanaoshiriki mapenzi na wenza wenye maambukizi ya fangasi hao.
Wanaolala kitanda kimoja na wenye maambukizi ya fangasi wa aina hii Wanaoshiriki mapenzi na wenza wenye maambukizi ya fangasi hao.
Eternal International Tuna Tiba (Virutubisho)Maalumu Yenye Uwezo Wa Kuondoa Magonjwa Ya Fangasi Wa Aina Zote. Tunapatikana Kinondoni-Morocco, Dar es salaam.
Pia tunatoa huduma ya vipimo vya mwili mzima (full body checkup) kwa ths 10,000/= tuu
Mawasiliano
0692428200
0765044875
0692385087 (Whatsapp)
0692428200
0765044875
0692385087 (Whatsapp)
@allyhamisi_ @allyhamisi_
NB:
BOFYA hapa CHINI kupata mfululizo wa makala yetu ya afya kila siku
Facebook page https://www.facebook.com/allyhamisi1225/
Whatsapp group https://chat.whatsapp.com/CwoN9qKG1wu6Rh8LgPTrxV
Instagram page @allyhamisi_ @allyhamisi_

No comments:
Post a Comment