Breaking

for more information click below

PropellerAds

Tuesday, 23 April 2019

WATOTO WA NYOTA YA MAPACHA


WATOTO WA NYOTA YA
MAPACHA
Watoto wa Nyota ya Mapacha ni wale waliozaliwa kati ya Tarehe 22 Mei mpaka tarehe 21 Mei
Watoto wa Nyota hii ni wachangamfu wanaopenda urafiki na ni rahisi sana kuwarubuni na kufikiwa kwa mtu yoyote. Kwa lugha nyingine watoto hawa wanacheka na mtu yoyote awe anamfahamu au asiyemfahamu. Wazazi wa watoto hawa mnatakiwa muwaelimishe sana watoto wenu kwani kuna hatari wanaweza wakarubuniwa na kuchukuliwa na mtu wasiyemfahamu.
Ni watoto wenye nguvu na bidii na wanapenda kujishughulisha na wakati mwingine inabidi uwalazimishe kulala.
Wazazi wa mtoto mwenye Nyota hii wanatakiwa wampe moyo wa kuwa na msimamo na juhudi ili mtoto huyu akamilishe malengo yake.
Watoto wa Nyota hii huwa wanapenda sana kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.anafanya jambo hili anaacha anafanya hili anaacha, matamano yao ni kama vile maji kupwa na maji kujaa.
Ni vizuri kwako wewe mzazi kumsistiza awe huru kuelezea jambo lake au anachokitaka.Watoto wa Nyota hii watakubali kupewa adhabu au kunidhamishwa kama ikiwa kuna sababu za kweli na umemuelezea akaelewa sababu ya wewe kumpa adhabu hiyo.
Tatizo kubwa utakalolipata wewe mzazi ni kumkuta mtoto huyu akifanya jambo ambalo hulipendi kwa sababu ni wajanja sana na hufanya mambo haraka haraka. Na ukimkamata atakuwa na majuto sana na atahakikisha huwezi kumkata tena. Wazazi wengi huwaona watoto hawa kama nusu malaika na nusu shetani.
Watoto hawa huwa wanapenda sana mijadala na kubishana na mwishowe hutokea ugomvi hasa na kaka zao au dada zao wale ambao yeye anawaona kama akili zao ni ndogo.
Wanauwezo wa kubadili maneno tena kwa uhakika mkubwa kiasi kwamba wewe mzazi ukashindwa kujua kama anayosema ni ya ukweli ama anadanganya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

PropellerAds