SAYARI YA IJUMAA VENUS-ZUHURA
Sayari hii iko Mbingu ya 3, Malaika wake anayeiangalia anaitwa Ann-yaill au Anael ambaye kazi yake ni kufanya doria Mbinguni. Jini anayetawala siku hii anaitwa Al abyadh au jina la utani anaitwa Abú Hassan Zoob’aa au Hagith.
Siku zake ni Ijumaa na Jumatatu usiku na nyota zake ni Mizani na Ng’ombe. au wenye majina yanayoanzia na G, S, B, N, Z
Sayari hii ni nyeupe na yenye kung’aa nayo inatembelea kila nyota katika muda wa siku 27 na inapitia kila sayari katika muda wa miezi 10. kwa maana ikikaa kwenye nyota yako mambo yanayokutokea yatakuwa yanahusiana na Sayari hii kama yalivyoainishwa hapa chini
Mafusho yake ‘Mustaka’ ambayo yako kama vijiwe vidogo vidogo vya rangi ya kijivu.
INAHUSIKA NA NINI
Sayari hii ya Venus au Zuhura inahusika na Muafaka, Urafiki, Uzuri wa moyo, Mapenzi, Masikilizano, Mapatano, Tabia nzuri, Mambo ya muziki, Starehe, Michezo na kila kitu chenye kufurahisha mwanamke.
FANYA YAFUATAYO
Siku ya Ijumaa ni siku nzuri ya kuoa, kuanza urafiki na mwanamke, kufanya tendo la ndoa, kusafiri, kufanya biashara, kupenda, mambo yote ya raha utakayofanya katika Siku hii ni mazuri na yenye baraka.
Leo uza vipodozi, uza nguo, uza vyombo vya muziki, anza kujenga nyumba, tengeneza gari, anza kupeleka watoto shule nk.
HAJA UTAPATA AU HUPATI
Leo Ijumaa ukiulizwa kama haja itapatikana , jibu kwamba ikiwa mwanzo wa siku Saa 12 hadi Saa 6 haja itapatikana tena hakuna vingine.
Ikiwa ni kati ya siku haja itapatikana baada ya uzito na taabu.
Ikiwa mwisho wa siku haja haipatikani milele
No comments:
Post a Comment