JE MAJINI WANAWEZA KUTUMIKA?
Majini wanaweza kutumika kwa kazi mbalimbali ambazo Binadamu anaweza kumtuma.
Mwenyezi Mungu aliwaamuru Majini wamtumikie Mfalme Suleimani na wakawa wanamfanyia Kazi kadri anavyotaka yeye.
Mwenyezi Mungu aliwaamuru Majini wamtumikie Mfalme Suleimani na wakawa wanamfanyia Kazi kadri anavyotaka yeye.
Katika Biblia 1 Wafalme 5: (13-17).
Biblia inaeleza jinsi nyumba ya Suleimani ilivyokuwa ikijengwa kimya kimya. ... “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwishachongwa chimboni, wala nyundo wala shoka, wala chombo cha chuma chochote sauti yake haikusikika ilipokuwa ikijengwa Nyumba”.
Majini vilevile wanatumiwa na watu katika kupata habari za mambo mbalimbali kwa sababu wao wana uwezo wa kupata habari angani.
Majini vilevile wanatumika katika ulinzi wa kulinda majumba au kulinda watu au Mikutano au Shughuli yeyote na vilevile wanaweza kutumika katika vita.
Wao wanajigeuza katika maumbo aidha ya Binaadamu au Mnyama na kushiriki katika vita.
Wao wanajigeuza katika maumbo aidha ya Binaadamu au Mnyama na kushiriki katika vita.
Mfano Shetani mmoja alijigeuza kwa mfano wa Binaadamu mmoja aitwae Saraqa Bin Malik na kushiriki vita vya Badri na kuwaahidi Makafiri ushindi mkubwa lakini alipoona Majeshi mawili ya Malaika wanateremka kutoka Mbinguni alitimka na kutoroka.
JE TUNAWEZA KUJIKINGA NA MASHETANI?
Zipo njia nyingi za kujikinga na Mashetani lakini kubwa zaidi ni kutumia Jina la Mwenyezi Mungu na kumtaka Mungu akuepushe na Shetani mbaya Naye atakusaidia.
Shetani ana Maudhi mengi sana kwa Binadamu kwa sababu anapenda kujishirikisha na Binadamu katika kila kitu kama vile katika kula, kunywa, kufanya Mapenzi, kutembea, Kuishi ndani ya Nyumba na hupenda kufanya hayo yote pale Mwanadamu anapopotea na kumsahau Mwenyezi Mungu.
Shetani vilevile anamgusa kila Mtoto anayezaliwa katika dunia hii. Mtoto ambaye hajaguswa na Shetani ni Yesu au Issa Bin Maryam hayo ni kwa mujibu wa maelezo ya Qurani na Mtume Muhammad (SAW).
Mashetani vilevile ndio wanasababisha Ugonjwa wa Tauni (Plague – Ugonjwa unaoambukiza). Mtume Muhammad (SAW) ameeleza “Hakika kuangamia kwa Umma wangu kunatokana na kushuka Hadhi yao na Ugonjwa wa Tauni na Adui yenu Mkubwa anatokana na Jini, na Hiyo kwenu ni Shahada”.
Hivyo basi ili kujiepusha na maovu ya Shetani unashauriwa kumweka mbele Mwenyeezi Mungu katika lolote unalolifanya ukiwa Nyumbani au popote pale.
Haya ni baadhi ya maelezo kuhusu Majini, zidi kutembelea tovuti hii mara kwa mara kwani hii ni mwanzo tu na tutazidi kuwaletea habari za ndani kuhusu majini na tabia zao, jinsi ya kujikinga nao au kushirikiana nao.
Marafiki na Maadui wa Majini
MARAFIKI WA MAJINI:
Majini huwa wanafanya Urafiki na Binadamu lakini Marafiki wao wakubwa ni Ngamia.
Baadhi yao wanaishi katika nyumba tunazoishi na ukitaka kuwafukuza unasoma Quran au Biblia au kumtaja Mwenyezi Mungu.
Baadhi yao wanaishi katika nyumba tunazoishi na ukitaka kuwafukuza unasoma Quran au Biblia au kumtaja Mwenyezi Mungu.
Majini hukusanyika na kuongezeka giza linapoingia au unapopatwa Mwezi, na huwa wanakimbia wanaposikia Adhana au Kengele ya kamba.
Majini wengi wanapenda kukaa baina ya kivuli na jua na siyo vizuri kukaa eneo hilo.
Majini wengi wanapenda kukaa baina ya kivuli na jua na siyo vizuri kukaa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment